Mkopo wa PAPO KWA PAPO (Papo2Papo) ni aina ya mkopo wa muda mfupi unaotolewa kwa mwanachama kwa lengo la kumwezesha kupata fedha kwa haraka ndani ya kipindi kifupi kilichoainishwa na Chama ili kukidhi mahitaji yake na kwa utaratibu rahisi, mchakato mwepesi na masharti mepesi ya mkopo kwa wakati muafaka.
Sifa za Mkopo:
1.     Kiwango cha juu cha mkopo huu hakitazidi shilingi milioni mbili (2,000,000/=)
2.     Muda wa marejesho hautazidi miezi sita (6)
3.     Kiwango cha riba ni asilimia moja (1%) kwa mwezi (Mstari myoofu)
4.     Mkopo huu hautegemei akiba alizonazo mwanachama
5.     Mkopo huu auhitaji wadhamini
Matukio yafuatayo yanaweza kuwa ni ya Papo2Papo kwa mwanachama
1.     Kupata msiba wa karibu wa familia ya mwanachama
2.     Tatizo la kuugua au kuuguliwa na mwanafamilia
3.     Mgogoro baina ya mwenye nyumba na mpangaji utakaopelekea mpangaji (mwanachama) kutaka kuondolewa katika nyumba hivyo kuhitaji fedha za haraka kwa ajili ya pango mpya
4.     Kulipa karo ya mtoto wa mwanachama ambaye yu karibu kusimamishwa masomo.
5.     Mwanachama kuibiwa, kuvunjiwa nyumba (Theft and Bulglary) na kuungua nyumba au kuteketezwa kwa moto
Utaratibu wa Mkopo wa Papo2Papo
1.     Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mwingine wa Papo2Papo endapo hatakuwa amekamilisha marejesho ya mkopo wa Papo2Papo uliotangulia
2.     Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa Papo2Papo hata kama ana mkopo mwingine kama vile mkopo wa maendeleo ya jamii au Emergency
Jinsi ya kurejesha Mkopo
Urejeshaji wa mkopo unaweza kufanyika kwa njia zifuatazo;
1.     Kukatwa kwenye Mshahara (Payroll Deduction)
2.     Makubaliano ya Kukatwa Benki (Bank Standing Order)
3.     Kupitisha mshahara kwenye JIKIMU Akaunti
4.     Kulipa Bank katika akaunti za Chama.
Jinsi ya kuomba
1.     Muombaji atahitajika kujaza fomu ya maombi na kuiwasilisha katika Ofisi ya Chama.
          Bofya hapa kupakua Fomu ya Maombi ya Mkopo.
Â
Â