Mkopo wa Maendeleo ya Jamii - (Social Development Loan – SDL) unatolewa kwa lengo la kumsaidia mwanachama katika kukidhi mahitaji yake ya kijamii kama vile:
1.     Karo za Shule/Chuo
2.     Ununuzi wa Samani (Furniture)
3.     Ujenzi na Umilikaji wa Nyumba
4.     Ununuzi wa Vyombo vya Moto
5.     Mtaji kwa ajili ya Biashara mbalimbali
6.     Mahitaji mengine yanayofanana na hayo yaliyotajwa hapo juu
Utaratibu wa mkopo wa maendeleo ya jamii
1.     Mkopo huu unatolewa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya muda mrefu ya mwanachama.
2.     Kiwango cha juu cha mkopo ni mara tatu (x3) ya Akiba ya Lazima (Compulsory Savings) ya mwanachama, lakini hautazidi TZS 150,000,000.
3.     Muda wa marejesho hautazidi miaka mitano (5), sawa na miezi 60. Marejesho yatategemea uwezo wa kulipa kwa kutumia makato ya mshahara au njia nyinginezo, bila kuathiri sheria mbalimbali zilizopo zinazomlinda mkopeshaji na mkopaji.
4.     Dhamana kwa mwanachama aliye ndani ya ajira ni:
·        Hisa
·        Akiba alizonazo
·        Pensheni yake
·        Wadhamini wawili (2)
5.     Dhamana kwa mwanachama aliye nje ya ajira ni:
·        Hisa
·        Akiba alizonazo
·        Wadhamini wawili (2)
·        Au mali nyingine zisizohamishika anazomiliki
6.     Riba ni asilimia nane (8%) kwa mwaka katika salio linalopungua (Reducing Balance Method).
7.     Mkopaji anaweza kupewa mkopo mwingine (Top Up) endapo marejesho sita (6) ya mkopo wa awali yameshafanyika.
Jinsi ya kurejesha mkopo
Urejeshaji wa mkopo unaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
1.     Kukatwa kwenye Mshahara (Payroll Deduction)
2.     Makubaliano ya Kukatwa Benki (Bank Standing Order)
3.     Kupitisha mshahara kwenye Akaunti ya JIKIMU
4.     Kulipa Benki katika akaunti za Chama
Â
Jinsi ya kuomba
1.     Muombaji atahitajika kujaza fomu ya maombi (TRASACCO-2) na kuiwasilisha katika Ofisi ya Chama.
          Bofya hapa kupakua Fomu ya Maombi ya Mkopo.
Â