SAFARI LOAN
Mkopo wa Likizo & Fungate
Lengo la Mkopo
Safari Loan ni bidhaa maalum ya mkopo inayomwezesha mwanachama kupata mkopo wa hadi mara mbili (x2) ya akiba yake ya Vacation Savings, ili kumsaidia kutimiza ndoto za:
-
Likizo
-
Fungate
-
Safari za mapumziko na burudani
-
Kutembelea maeneo ya ndoto yake, ndani na nje ya nchi
Masharti ya Mkopo
-
Kiasi cha Mkopo
-
Mwanachama atakopeshwa hadi mara mbili (x2) ya akiba yake ya Vacation Savings.
-
-
Riba ya Mkopo
-
Riba ya 8% kwa mwaka, itakayokokotolewa kwenye salio halisi la mkopo.
-
-
Muda wa Marejesho
-
Marejesho ya mkopo yatakuwa kwa kipindi kisichozidi miezi 18.
-
-
Njia za Marejesho
-
Marejesho yatafanyika kupitia:
-
Makato ya mshahara, au
-
Bank Standing Order itakayowekwa kwenye Akaunti ya Jikimu ya mwanachama.
-
-
-
Masharti Mengine
-
Masharti mengine yote ya mkopo yatafuata Sera ya Mikopo ya TRA SACCOS inayotumika.
-
Faida Kuu za Safari Loan
-
Unatimiza ndoto za kusafiri bila kusubiri muda mrefu
-
Riba nafuu ya 8%
-
Mkopo wa haraka unaotegemea akiba yako mwenyewe
-
Muda mfupi wa marejesho (hadi miezi 18)
-
Unaweza kusafiri popote ulipo ndoto yako
Muhtasari wa Mkopo
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Aina ya Mkopo | Safari Loan |
| Riba | 8% |
| Muda wa Mkopo | Hadi miezi 18 |
| Kigezo Kikuu | Akiba ya Vacation Savings |
| Kiasi cha Mkopo | Hadi x2 ya akiba |
| Njia ya Marejesho | Mshahara / Standing Order |
| Kiasi cha Juu | TZS 50,000,000/= |
Timiza Ndoto ya Safari Yako Leo!
Pata Safari Loan kwa masharti rafiki, riba nafuu na marejesho mafupi – safari yako inaanza hapa.