Ni akaunti maalum ya akiba inayomuwezesha mwanachama kuwekeza fedha zake kwa nidhamu na mpango wa muda maalum bila kuzitoa kwa kipindi cha kuanzia miaka mitatu (3). Akaunti hii imeundwa kwa lengo la kumsaidia mwanachama kukuza mtaji wake kwa uhakika huku akipata faida ya riba kila mwaka.
Ni suluhisho bora kwa mwanachama anayehitaji kuwekeza kwa malengo ya muda wa kati kama vile kuanzisha biashara, kununua kiwanja, kujenga nyumba au kujiandaa na mahitaji makubwa ya kifedha yajayo.
Faida za Akaunti ya Wekeza
-
Fursa ya Uwekezaji wa Muda Maalum
Mwanachama anapata nafasi ya kuwekeza fedha zake kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mpango maalum wa kukuza akiba. -
Riba ya 7% kwa Mwaka
Riba ya asilimia saba (7%) hulipwa kila mwaka mara tu mwanachama anapofikisha angalau TZS 500,000 katika akaunti yake. -
Uhuru wa Kuchagua Matumizi ya Riba
Mwanachama anaweza kuchagua: -
Kulipwa riba yake moja kwa moja, au
-
Kuendelea kuiwekeza katika akaunti ya Wekeza ili kuongeza mtaji wake (Chaguo la kwanza: faida itaongezwa moja kwa moja kwenye akaunti ya WEKEZA).
-
Muda wa Uwekezaji – Miaka 3
Kipindi rasmi cha uwekezaji ni miaka mitatu (3). -
Kuendeleza Uwekezaji (Renewal Option)
Baada ya kukamilika kwa miaka mitatu ya kwanza, mwanachama anaweza kuhuisha na kuanza kipindi kingine cha miaka mitatu. -
Urahisi wa Kuchangia
Mwanachama anaweza kuweka fedha: -
Kupitia mshahara
-
Kwa kuweka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za chama
-
Kupitia makubaliano ya Bank Standing Order
-
Inaweza Kutumika kama Dhamana ya Mkopo
Salio la akaunti ya Wekeza linaweza kutumika kama dhamana ya kupata mkopo ndani ya chama.
Â
Vigezo na Masharti
-
Ili kupata riba kamili ya 7% kwa mwaka, mwanachama hataruhusiwa kutoa fedha katika akaunti hii kwa kipindi chote cha miaka mitatu (3).
-
Endapo mwanachama ataamua kuchukua sehemu au fedha zote kabla ya kipindi kuisha, atalipwa nusu (½) ya riba iliyopatikana kwa mwaka au miaka iliyopita.
Masharti haya yanasaidia kuhakikisha uwekezaji unalindwa na unaleta faida iliyokusudiwa.
Â
Akaunti za Benki za Chama
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
-
NBC: 012103020266
-
CRDB: 01J1328947802
-
NMB: 20310008081
-
AZANIA: 00100021049
Wanachama wanaweza kutumia akaunti hizi kuweka michango yao ya Wekeza.
Â
Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Wekeza
-
Bofya hapa kufungua fomu ya maombi.
-
Jaza fomu kikamilifu kwa taarifa sahihi.
-
Pakua hati ya maombi katika mfumo wa PDF.
-
Tuma fomu hiyo kupitia barua pepe ya Chama:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Â