Â
Vacation Savings ni mfuko maalum wa akiba unaomuwezesha mwanachama kujiwekea fedha kwa ajili ya ndoto zake za safari, ikiwa ni pamoja na:
- Safari nje ya nchi
- Kutembelea vivutio vya utalii ndani ya nchi
- Safari za mapumziko na burudani kama Likizo / Fungate / Hija
Bidhaa hii inasaidia mwanachama kupanga safari zake mapema, bila msongo wa kifedha, na kuhakikisha akiba yake inakuwa salama huku ikizalisha riba.
 Masharti ya Akiba
1. Kiasi cha Akiba
- Michango ya kila mwezi kuanzia TZS 50,000 au zaidi.
2. Njia za Uchangiaji
- Bank Standing Order
- Kukatwa moja kwa moja kwenye mshahara
3. Urahisi wa Kutoa Akiba
- Mwanachama anaweza kutoa sehemu au akiba yote wakati wowote bila kufunga akaunti.
- Akiba hii inaweza pia kutumika kama dhamana ya Mkopo wa Safari (Safari Loan).
4. Kiwango cha Riba
- Riba ya uhakika ya 3% kwa mwaka.
5. Uwezo wa Kukopa
- Akaunti ya Vacation Savings humwezesha mwanachama kupata Safari Loan hadi mara mbili (x2) ya akiba yake.
Â
Faida Kuu za Vacation Savings
- Inakuwezesha kupanga likizo mapema bila presha
- Akiba salama yenye riba ya uhakika
- Inakupa fursa ya kupata Safari Loan kwa urahisi
- Hakuna kufunga akaunti ili kutoa akiba
Â
Muhtasari wa Bidhaa
|
Kipengele |
Maelezo |
|
Akiba ya Kuanzia |
TZS 50,000/= |
|
Riba |
3% kwa mwaka |
|
Utoaji wa Akiba |
Wakati wowote |
|
Mkopo Unaohusiana |
Safari Loan |
|
Kiwango cha Mkopo |
Hadi x2 ya akiba |
Â
Akaunti za Benki za Chama
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
- NBC: 012103020266
- CRDB: 01J1328947802
- NMB: 20310008081
- AZANIA: 00100021049
Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Maandalizi ya Kustaafu
- Bofya hapa kufungua fomu ya maombi.
- Jaza fomu kwa taarifa sahihi.
- Pakua hati ya maombi katika mfumo wa PDF.
- Tuma fomu hiyo kupitia barua pepe ya Chama:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Â
Hitimisho
Jiwekee Akiba ya Safari na Mapumziko kwa Urahisi na Riba ya Uhakika!
Anza leo na uweke mpango mzuri wa kifedha ili ndoto zako za kusafiri zitimie bila msongo wa kifedha.
Â