Akiba ya Lazima (Compulsory Savings ) ni mchango wa lazima kwa kila mwanachama wa TRA SACCOS. Akaunti hii humjengea mwanachama msingi imara wa kifedha na hutumika kama dhamana muhimu ya kupata mikopo mbalimbali ndani ya Chama.

Akiba hii ni sehemu ya uwajibikaji wa uanachama na ni chachu ya maendeleo ya kifedha ya mwanachama.

Faida za Compulsory Savings

  1. Huzalisha Riba Kila Mwaka
    Akiba yako huzalisha faida ya riba (Interest on Savings) kila mwaka, hivyo kuongeza thamani ya mchango wako.
  2. Huongeza Uwezo wa Kupata Mkopo Mkubwa
    Kadri akiba yako inavyoongezeka, ndivyo kiwango cha mkopo unachoweza kupata kinavyoongezeka.
  3. Ni Dhamana ya Mikopo
    Compulsory Savings hutumika kama sehemu ya dhamana ya mikopo unayoomba ndani ya SACCOS hususani Mkopo wa maendeleo ya Jamii,ambao unakopa X3 ya akiba yako.
  4. Hujenga Nidhamu ya Kuweka Akiba
    Inamsaidia mwanachama kuwa na utaratibu endelevu wa kuweka akiba na kujijengea usalama wa kifedha.

 Kiwango cha Chini cha Mchango

  • Kiwango cha chini cha Compulsory Savings ni TZS 100,000 kwa mwezi.

Mchango huu unaweza kufanyika kupitia:

  • Makato ya mshahara
  • Kuweka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za Chama
  • Makubaliano ya Bank Standing Order

Akaunti za Benki za Chama

Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD

  • NBC: 012103020266
  • CRDB: 01J1328947802
  • NMB: 20310008081
  • AZANIA: 00100021049

Hitimisho

Compulsory Savings ni nguzo ya uanachama na maendeleo ya kifedha ndani ya SACCOS. Kwa kuweka angalau TZS 100,000 kila mwezi, unajenga msingi wa kupata mikopo mikubwa na kukuza ustawi wako wa kifedha.

Wekeza kwa nidhamu, fanikiwa kwa uhakika.

Â