Sababu za Kuanzishwa kwa Akiba ya Tajirika
Kwa kipindi kirefu, wanachama wa TRA SACCOS LTD walikuwa na shauku ya kutumia hati fungani (bonds) zao kama dhamana ya kupata mikopo yenye riba nafuu kupitia Chama chao.
Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa ukwasi (liquidity) ndani ya Chama, utekelezaji wa ombi hilo ulikuwa changamoto kubwa.
Kutambua hitaji hili, na kwa lengo la:
- Kukidhi mahitaji ya wanachama, na
- Kulinda ustawi na uendelevu wa Chama,
Bodi ya Wakurugenzi wa TRA SACCOS LTD imebuni bidhaa maalum ya akiba iitwayo Tajirika Savings (Akiba ya Tajirika). Bidhaa hii inalenga kuongeza ukwasi wa Chama huku ikiwwezesha wanachama kutumia hati fungani zao kupata mkopo wa riba nafuu.
Maelezo ya Akiba ya Tajirika
Akiba ya Tajirika ni akiba maalum inayolenga:
- Kukuza kipato cha mwanachama
- Kujenga nidhamu ya kifedha
- Kuwezesha mafanikio ya kifedha ya muda mrefu
Sifa Kuu za Akiba ya Tajirika
- Kianzio cha Akiba
Kuanzia TZS 50,000. - Gawio
Riba ya asilimia 3% kila mwaka, ikikua na muda na akiba yako. - Uwezo wa Kukopa
Hukuwezesha kupata Bond Loan hadi mara tatu (3x) ya thamani ya Akiba ya Tajirika uliyoweka. - Usalama wa Akiba
Akiba inalindwa na kusimamiwa kwa mujibu wa sera na miongozo ya TRA SACCOS LTD.
Faida kwa Mwanachama
- Upatikanaji wa mkopo wa riba nafuu kupitia Bond Loan
- Akiba yenye gawio la uhakika kila mwaka
- Fursa ya kupanga na kutimiza malengo ya kifedha ya muda mrefu
- Kuchangia ukuaji na uimara wa Chama
Â
Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Akiba ya Tajirika
- Bofya hapa kufungua fomu ya maombi.
- Jaza fomu kwa taarifa sahihi.
- Pakua hati ya maombi katika mfumo wa PDF.
- Tuma fomu hiyo kupitia barua pepe ya Chama:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Akaunti za Benki za Chama
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
- NBC: 012103020266
- CRDB: 01J1328947802
- NMB: 20310008081
- AZANIA: 00100021049
Hitimisho
Akiba ya Tajirika ni suluhisho endelevu kwa mwanachama anayehitaji:
- Ukuaji wa kifedha
- Mkopo wa riba nafuu
- Akiba salama ndani ya Chama chake
Wekeza leo, Tajirika kesho!
Â