Lengo la Mkopo
Mkopo wa Jipange(Jipange Loan) ni bidhaa maalum ya mkopo inayolenga kumwezesha mwanachama kupanga maisha yake, miradi na uwekezaji kwa kutumia akiba zake mwenyewe kama msingi wa kupata mkopo, bila mzigo mkubwa wa riba.
Masharti ya Mkopo
-
Uwepo wa Akiba Husika
-
Mwombaji wa mkopo lazima awe na mfuko wa akiba ya Wastaafu na/au Wekeza unaoendelea.
-
-
Njia ya Kupokea Mkopo
-
Mkopo utatolewa kupitia Akaunti ya Jikimu ya mwanachama.
-
-
Marejesho ya Mkopo
-
Marejesho yatalipwa kupitia:
-
Mshahara, au
-
Standing Order kwa wanachama wanaopitisha mishahara yao kupitia Akaunti ya Jikimu.
-
-
-
Kiwango cha Juu cha Mkopo
-
Mkopo hautazidi mara mbili (x2) ya akiba ya Wastaafu na/au Wekeza.
-
-
Ustahiki wa Mkopo
-
Mwombaji mwenye malimbikizo ya marejesho ya mkopo mwingine hataruhusiwa kukopesheka.
-
-
Muda wa Marejesho
-
Marejesho ya mkopo hayatazidi miezi 36.
-
-
Riba ya Mkopo
-
Riba ya 12% kwa mwaka, itakayokokotolewa kwenye salio la mkopo.
-
Kiwango hiki kinazingatia kuwa mwanachama tayari anapata riba ya 7% kwa mwaka kwenye akiba zake za Wekeza/Wastaafu.
-
Faida Kuu za Jipange Loan
-
Unatumia akiba yako kama nguvu ya kukuwezesha kukopa
-
Inakusaidia kupanga miradi na uwekezaji kwa uhakika
-
Riba iliyopimwa kwa kuzingatia faida ya akiba zako
-
Muda rafiki wa marejesho hadi miezi 36
-
Mkopo rahisi unaopitia Akaunti ya Jikimu
Muhtasari wa Mkopo
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Aina ya Mkopo | Jipange Loan |
| Walengwa | Wanachama wenye Akiba ya Wastaafu/Wekeza |
| Riba | 12% |
| Muda wa Mkopo | Hadi miezi 36 |
| Kiasi cha Juu | Hadi x2 ya Akiba (≤ TZS 50,000,000/=) |
| Njia ya Marejesho | Mshahara / Standing Order |
| Akaunti | Jikimu |
Panga Maisha Yako Leo, Jipange Kesho Yako
Jipange Loan ni mkopo unaotumia akiba yako kukuinua zaidi katika maisha na uwekezaji.
Jinsi ya Kuomba Mkopo