Akaunti ya Akiba ya Elimu ni akaunti maalum inayomuwezesha mwanachama kuchangia kwa hiari ili kujiandaa na gharama za elimu. Akaunti hii imekusudiwa kusaidia kulipa karo za shule au chuo kwa ajili ya mwanachama mwenyewe, ndugu au wategemezi wake.

Ni njia salama na yenye mpango wa kuhakikisha mahitaji ya elimu yanatimizwa kwa wakati bila msongo wa kifedha.

Faida za Akaunti ya Akiba ya Elimu

  1. Huzalisha Riba Kila Mwaka
    Akiba yako itazaa faida ya Interest on Savings kila mwaka, hivyo kukuza mtaji wako wa elimu.
  2. Mkopo wa Elimu Mara Mbili ya Akiba
    Mwanachama anaweza kupata Mkopo wa Elimu unaofikia hadi mara mbili (2) ya kiasi cha Akiba ya Elimu alichokusanya.
  3. Urahisi wa Kupunguza Akiba
    Unaweza kupunguza Akiba ya Elimu hadi mara nne (4) kwa mwaka (kila robo mwaka mara moja), mradi tu kiasi kinachopunguzwa hakiathiri dhamana ya Mkopo wa Elimu.
  4. Malipo ya Haraka
    Endapo mwanachama atahitaji kupunguza kiasi cha akiba, malipo hufanyika ndani ya masaa 24 kupitia Simu au Benki.
  5. Urahisi wa Kuchangia
    Mwanachama anaweza kuweka akiba kupitia:
    • Makato ya mshahara
    • Kuweka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za Chama
    • Makubaliano ya Bank Standing Order

Vigezo na Masharti

  • Kiwango cha chini cha kuweka ni TZS 100,000.

Akiba hii ni ya hiari na inamwezesha mwanachama kupanga michango yake kulingana na uwezo wake wa kifedha.

Akaunti za Benki za Chama

Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD

  • NBC: 012103020266
  • CRDB: 01J1328947802
  • NMB: 20310008081
  • AZANIA: 00100021049

Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Akiba ya Elimu

  1. Bofya hapa kufungua fomu ya maombi.
  2. Jaza fomu kwa usahihi.
  3. Pakua hati ya maombi katika mfumo wa PDF.
  4. Tuma fomu hiyo kupitia barua pepe ya Chama:
    This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Hitimisho

Akiba ya Elimu ni suluhisho bora kwa mwanachama anayejali mustakabali wa elimu. Kwa riba ya kila mwaka, uwezekano wa kupata mkopo mara mbili ya akiba yako, na urahisi wa kupunguza akiba kwa wakati wa mahitaji — akaunti hii inakupa uhakika wa kupanga na kutimiza malengo ya elimu kwa utulivu.

Anza kuwekeza leo kwa elimu ya kesho.

Â